1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush aahidi kuunga mkono uanachama wa Ukraine na Georgia katika NATO.

1 Aprili 2008
https://p.dw.com/p/DYqj

Kiev.

Rais wa Marekani George W. Bush ameahidi kuunga mkono nia ya Ukraine na Georgia kujiunga na NATO licha ya upinzani kutoka Russia.

Baadhi ya wanachama wa jumuiya hiyo kutoka mataifa ya Ulaya pia wanapinga upanuzi wa NATO kuelekea upande wa mashariki.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na rais wa Ukraine Viktor Yushchenko mjini Kiev, Bush amesema atashinikiza washirika wake wa mataifa ya magharibi katika mkutano wa wiki hii wa NATO nchini Romania kuunga mkono hatua hiyo ya mpango wa uanachama kwa mataifa ya Ukraine na Georgia.

Rais wa Marekani pia amejaribu kuondoa wasi wasi wa Russia kuhusu ombi la Ukraine kujiunga na NATO pamoja na ngao ya ulinzi dhidi ya makombora ambayo Marekani inapanga kuweka nchini Poland na jamhuri ya Chek.

Bush , ambaye anaizuru Ukraine kabla ya mkutano wa siku tatu wa NATO utakaofanyika mjini Bucharest nchini Romania , alilakiwa na waandamanaji wanaoipinga NATO.