1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush asema Iran ndio inaongoza kwa kuunga mkono ugaidi dunaini

13 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cp3G

ABU-DHABI:

Rais George W.Bush amewaomba washirika wa Marekani katika eneo la Ghuba la Uajemi kukabiliana na Iran.

Katika hotuba yake mjini Abu Dhabi, rais Bush amesema kuwa Iran ndio inaongoza nchi zote duniani kwa kuunga mkono ugaidi.

Asema kuwa Iran inaunga mkono ugaidi duniani kwa kutoa mamilioni ya pesa huku wananchi wake wanateseka kwa umaskini.Aidha amesema kuwa Iran inazuzuia usalama kurejea nchini Lebanon kwa kuliunga mkono kundi la Hezbullah.

Pia ameishutumu Iran kwa kuunga mkono kundi la Wapalestina la Hamas pamoja na wapiganaji wa chini kwa chini wa Kishia nchini Iraq. Ziara ya Bw Bush katika Umoja wa Falme za kiarabu ni kituo cha tatu cha ziara yake katika eneo la Mashariki ya kati.Lengo la safari yake hii ni kujaribu kuomba uungwaji mkono wa juhudi za kupatikana kwa mkataba wa amani kati ya wapalestina na waisrael usainiwe kabla ya muhula wake kumalizika katika mda wa mwaka mmoja kutoka sasa.Kutoka huko Bw Bush ataelekea Saudi Arabia na kukamilisha ziara yake hii ya siku nane nchini Misri.