1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush hapangi kuondoa majeshi Irak

11 Aprili 2008

Rais George Bush wa Marekani hana azma ya kuondoa majeshi zaidi kutoka Irak na aionya Iran.

https://p.dw.com/p/Dg2O
George Bush (kulia)Picha: AP

Rais George Bush wa Marekani, hana mpango wa kuyarejesha nyumbani haraka majeshi ya Marekani kutoka Irak.Alisema hayo jana mjini Washington.Kwa matamshi hayo amechochea mjadala motomoto nchini kuhusu muelekeo wa sera ya Marekani ya siku zinazokuja juu ya Irak.

Buish hana mengi ya kuwaeleza wamarekani waliochoshwa mno na vita hivi vya Irak. Aliwaambia tu kwamba hana dhamiri ya kupunguiza zaidi majeshi mbali na ile idadi ya askari 30.000 iliotangazwa kabla.Badala yake,atapitisha kipindi cha siku 45 mwishoni mwa Julai cha kuwaza .Mwishoni mwa muda huo, yatarajiwa hali itabakia vile vile kama alivyopendekeza Amirijeshi mkuu wa Marekani nchini Irak-jamadari Petraeus. kikosi cha kiasi askari 140,000 kitabakia Irak kwa muda usiojulikana.

Kwa kikoosi hicho , anatumai amirijeshi mkuu huyo nafuu kidogo:

"Ili kuwarahisishia kazi ,nimeamrisha kutoka sasa mtatumika miezi 12 badala ya mwaka nchini Irak."

Alisema Bush.

Hata ikiwa hatua yake ya mwaka mmoja uliopita ya kuongeza majeshi nchini Irak imeleta usalama zaidi kwa aonavyo yeye,hali ya mambo haiko vile ambavyo angependelea iwe.Kwa muujibu wa jamadari Petraues,Iran inawasaidia waasi nchini Irak katika vita vyao dhidi ya Marekani.Kwahivyo, rais Bush ameitaka Iran kuacha kutoa msaada huo.

"Endapo Iran ikichukua uamuzi usio barabara,Marekani itaichukulia hatua ili kulinda tangu masilahi yake, wanajeshi na mshirika wake."

Alitishia Bush.

Yote hayo hayatoi ishara kwamba vita vya Irak vinakaribia kumalizika-vita ambavyo sehemu kubwa ya wamarekani wamechoshwa navyo na hata watetezi 2 wa chama cha democrat kwa wadhifa wa urais Hillary Clinton na Barack Obama wanavipinga vikali.

"Hata ikiwa vita hivi vigumu,havitaselelea daima.Tunatarajia hali ya mambo itaendelea kutengenea na kila tukifanikiwa tutawarejesha wanajeshi zaidi nyumbani."

Wademokrat hawaamini hayo na wanamjibu kwa kutoa hata ila kali zaidi juu ya hotuba ya jana ya George Bush.Wanamtuhumu kwamba hapangi kabisa mwisho wa majeshi ya Marekani kubakia Irak wala kulitatua tatizo la Irak.Bush anataka kumuachia mzigo wa vita vya Irak, rais atakaeshika madaraka baada yeye kuondoka.