1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush-London

Ali, Ramadhan15 Juni 2008

Rais G.Bush wa Marekani atakutana kesho na waziri mkuu G.Brown kwa mazungumzo.

https://p.dw.com/p/EK1D
RaisG.Bush akiaga barani Ulaya.Picha: AP


Rais George Bush wa Marekani anaelekea leo London,Uingereza akiwa katika hatua yake ya mwisho ya ziara yake ya kuaga barani Ulaya.Wakati wa ziara hii,rais Bush ametumia wakati mwingi kujaribu kuunda safu moja ya kuishinikiza Iran kusimamisha kabisa mradi wake wa kurutubisha madini ya uranium.

Ujerumani,Itali na Ufaransa zote zimemuunga mkono.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani,alifika hata kuunga mkono vikwazo zaidi dhidi ya Iran ikiwa itakataa kuupokea mkono mpya wa mapendekezo ilionyoshewa na dola kuu ili iaachane na mradi huo.


Rais George Bush akiwa Ufaransa jana alionya:

"Iran yenye silaha za kinuklia,inaleta hali ya misukosuko na nahisi itakua pigo kubwa kwa amani ya ulimwengu.Hivyo,nimevunjwa moyo kwa viongozi wake wameukataa mkono karimu walionyosewa."


Rais George Bush anatazamiwa kuwa na mazungumzo na waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown, kesho Jumatatu kabla ya kurejea nyumbani Washington.