1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Bush -Sarkozy waujadili mzozo wa fedha

19 Oktoba 2008
https://p.dw.com/p/Fcw4

Camp David:

Marekani na Umoja wa Ulaya zimekubaliana kuandaa mlolongo wa mikutano ya kilele ya kimataifa kuhusu mzozo wa fedha duniani. Uamuzi huo ulitangazwa baada ya Rais George W.Bush wa Marekani kukutana na mwenzake wa Ufaransa Nikolas Sarkozy na mkuu wa Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barroso huko Camp David-Marekani.Viongozi hao walikubaliana kwamba Marekani iwe mwenyeji wa mkutano wa kwanza utakaofanyika baada ya uchaguzi wa Rais wa Marekani tarehe 4 mwezi ujao wa Novemba. Mkutano huo utazingatia juu ya msingi ya marekebisho katika mfumo wa fedha wa kimataifa, na ile itakayofuata itatathmini hatua nyengine muwafaka. Bw Sarkozy na Barroso wanataka paweko na marekebisho makubwa ya fedha duniani kufuatia msukosuko huu wa sasa ambao ni mbaya kabisa tangu miaka ya 1930.