1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 kuanza Julai

20 Februari 2024

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limefikia makubaliano kuhusu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika itakayotimua vumbi mwezi Julai na Agosti mwaka ujao wa 2025 nchini Morocco.

https://p.dw.com/p/4cdD3
Patrice Motsepe
Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe Picha: Wikus de Wet/AFP/Getty Images

Tarehe zinazopendekezwa ni kuanzia Julai 20 hadi 16 au 17 Agosti mwaka 2025.

Mapema mwezi huu rais wa CAF Patrice Motsepe alikataa kuthibitisha tarehe za michuano hiyo, huku wenyeji wakiwa na muda mchache wa kuandaa mashindano ya kuwania kufuzu kama michuano hiyo ingepangwa kufanyika Januari na Februari mwakani.

Hata hivyo, kuchezwa kwa mechi za Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Juni na Julai mwaka ujao, kutamaanisha kuwa michuano hiyo itafanyika sambamba na michuano iliyotanuliwa ya Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA ambayo inatarajiwa kufanyika huko Amerika Kaskazini.

Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika ya mwaka 2027 itaandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania.