1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Adhabu ya jela kwa kukataa kulinda ubalozi wa Israel

25 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCOd

Mahakama ya polisi nchini Misri imetoa adhabu ya kifungo cha miezi sita kwa afisa wa polisi aliekataa kulinda ubalozi wa Israel katika mji mkuu wa Misri,Cairo.Mohamed Khalaf Hassan Ibrahim alikuwa hospitali katika mgomo wa chakula, akipinga kuwekwa kizuizinilakini hii leo aliweza kuhudhuria kikao cha mahakamani.Vikosi vya polisi nchini Misri huendeshwa sawa na majeshi,kwa hivyo kama ilivyo na mahakama ya kijeshi,hakuna uwezekano wa kukata rufaa.Misri,katika mwaka 1979,ilikuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu kutia saini mkataba wa amani na Israel.