1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Al Qaider watoa wito kwa wasomali kupigana jihad

26 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFL

Mpiganaji wa kundi la Al Qaider aliyetoroka kutoka katika mikono ya Marekani huko Afghanistan mwaka 2005 ametoa wito kwa wanamgambo wa kisomali kupigana vita takatifu ya jihadi dhidi ya majeshi ya serikali ya mpito ya Somalia.

Katika taarifa yake kupitia mkanda wa video, Abu Yahia al Lipi, amewataka mujahidina wa Somalia kupigana vita ya mtaani dhidi ya majeshi ya serikali akisema ni vita tamu kwa kundi la watu wa chache na inayochukua muda mrefu.

Wiki iliyopita Abu Yahia alitoa taarifa kupitia mkanda wa video akiwataka wanamgambo wa kisunni nchini Iraq kuuangana pamoja chini ya uongozi wake kupambana na majeshi ya Marekani aliyosema yameshindwa.

Wakati huo huo viongozi wa koo kubwa nchini Somalia wamesema kuwa makubaliano ya kusitisha mapiganao kati yao na majeshi ya Ethiopea yanaendelea.

Hiyo inafuatia mazungumzo kati ya koo hizo na majeshi ya Ethiopea yanaunga mkono serikali ya mpito ya Somalia, baada ya mapigano wiki iliyopita yaliyopelekeka watu 20 kuawa.

Mkuu na msemaji wa Hawiye,Ahmed Diriye Diriye, pia amesema kuwa mpango wa kuwanyang´anya silaha watu umesitishwa kufuatia makubaliano hayo.