1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO : Kansela Merkel akutana na Rais Mubarak

4 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVK

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ameanza ziara yake ya siku nnne Mashariki ya Kati kwa lengo la kutafuta njia za kufufuwa mchakato wa amani uliokwama kati ya Israel na Wapalestina.

Kansela Merkel amelifanya suala hilo kuwa mojawapo ya kipau mbele cha juu cha sera ya kigeni ya Ujerumani wakati nchi hiyo ikishikilia wadhifa wa Urais wa Umoja wa Ulaya na ule wa Kundi la Mataifa Manane yenye Maendeleo ya Viwanda Duniani.

Kituo chake cha kwanza cha ziara hiyo ni Cairo ambapo amekutana na Rais Hosni Mubarak wa Misri.Kufuatia mazungumzo yao viongozi hao wawili wamesema wamekubaliana juu ya haja ya kushirikisha wanachama wengi zaidi kadri inavyowezekana wa jumuiya ya kimataifa katika suala la kuleta amani Mashariki ya Kati.

Merkel pia anatazamiwa kuitembelea Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kirabu na Kuwait katika ziara yake hiyo.