1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Kansela wa Ujerumani ziarani Mashariki ya Kati

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVX

Kansela wa Ujerumani,Angela Merkel hii leo anaanza ziara yake ya siku nne katika Mashariki ya Kati.Kituo cha kwanza ni Cairo,ambako atakutana na rais Hosni Mubarak wa Misri.Wakati wa ziara yake,Kansela Merkel atajitahidi kufufua mazungumzo ya amani ya Mashariki ya Kati yaliokwama.Suala hilo ni miongoni mwa vipaumbele vya siasa yake ya kigeni,wakati huu ambapo Ujerumani imeshika nyadhifa za urais katika Umoja wa Ulaya na kundi la nchi tajiri zilizoendelea kiviwanda G-8.Merekel pia anatazamia kuzungumza juu ya migogoro ya hivi sasa kuhusu Lebanon na mradi wa kinuklia wa Iran.Ziara ya Kansela Merkel itampeleka pia nchini Saudi Arabia,Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE na Kuwait.