1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Marekani imelaumiwa kuhusu mswada wa Israel

12 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtU
Umoja wa nchi za Kiarabu,umelaumu vikali msimamo uliochukuliwa na Marekani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.Marekani imetumia kura yake ya turufu katika Baraza la Usalama, dhidi ya mswada wa azimio uliowasilishwa na Qatar kwa niaba ya nchi za Kiarabu.Mswada huo umetoa mwito kuilaumu Israel kwa shambulio lililofanywa na vikosi vyake katika mji wa Beit Hanoun kwenye Ukanda wa Gaza.Shambulio hilo liliua Wapalestina 18-wengi wao walikuwa wanawake na watoto.