1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cairo. Misr iko tayari kuchangia wanajeshi.

29 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC62

Misr imeufahamisha umoja wa mataifa kuwa iko tayari kuchangia wanajeshi mia kadha kama sehemu ya jeshi la umoja wa mataifa ili kuimarisha jeshi la kulinda amani la Afrika katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Waziri wa mambo ya kigeni Ahmed Aboul Gheit amesema katika taarifa iliyopokelewa jana Jumamosi kuwa Misr imetoa ahadi ya kuchangia zaidi ya wanajeshi 500 , pamoja na wataalamu 200 hadi 300 wa masuala ya kiufundi kama ishara na usafiri , wachunguzi 100 na maafisa 30.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Misr iko tayari kuangalia uwezekano wa kuongeza wanajeshi zaidi. Lakini Sudan haijaidhinisha jeshi la umoja wa mataifa litakalokuwa pamoja na lile la umoja wa Afrika litakalokuwa na wanajeshi 20,000 na polisi, ambalo baraza la usalama limeidhinisha mwezi August mwaka jana.