1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cairo. Misr kufanya mabadiliko katika katiba.

21 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGz

Rais wa Misr Hosni Mubarak ametangaza kufanyika kwa kura ya maoni hapo March 26 kuhusiana na suala tete la mabadiliko ya katiba yaliyopitishwa bungeni.

Wanasiasa wa upinzani wameshutumu kura hiyo ya maoni, wakisema kuwa mageuzi yanayopendekezwa katika katiba yanatishia uhuru wa raia.

Mabadiliko hayo ni pamoja na vifungu vinavyohusu mapambano dhidi ya ugaidi ambavyo vitawapa mamlaka polisi ya kukamata watu pamoja na uchunguzi.

Mabadiliko hayo pia yatamruhusu rais kulivunja bunge na yatadhoofisha njia za kisheria za kushughulikia chaguzi. Makundi ya upinzani yanafikiria kususia kura hiyo.