1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Msichana amefariki Misri kwa virusi vya H5N1

9 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtK

Nchini Misri mtoto aliekuwa akiumwa homa ya mafua ya ndege amefariki dunia.Kwa mujibu wa msemaji wa wizara ya afya,siku ya Alkhamisi,matokeo ya uchunguzi uliofanywa,yalithibitisha kuwa msichana huyo wa miaka 10 alikuwa na virusi vya H5N1 ambavyo ni hatari kwa binadamu.Katika mwezi wa Februari nchini Misri,watu 35 waliugua homa hiyo na 15 walifariki.