1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Polisi wavunja maandamano ya upinzani

16 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCIj

Nchini Misri,polisi wamevunja maandamano ya kuipinga serikali yaliyofanywa katika mji mkuu Cairo.Vile vile wamekamata si chini ya wanaharakati 30 wanaogombea demokrasia.Baadhi kubwa ya waandamanaj,walikuwa wafuasi wa Chama cha Kitaifa cha Mageuzi-Kefaya.Waandamanaji hao wameulaani mpango wa Rais Hosni Mubarak wa kutaka kuibadilisha katiba.Wapinzani wanadai kuwa mageuzi hayo yatapunguza uhuru nchini humo.