1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Rice asema Sudan lazima ikubali wanajeshi wa Umoja wa Mataifa

4 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD6N

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Bi Condoleezza Rice amesema Sudan lazima ikubali wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kwenda kulinda amani katika jimbo la Darfur.

Katika mkutano na waandishi habari mjini Cairo Misri, Condoleezza Rice amesema jeshi la Umoja wa Afrika halina uwezo wa kukabiliana na changamoto kubwa na kuliokoa eneo la Darfur na linatakiwa liondoke ili nafasi yake ichukuliwe na jeshi kubwa la Umoja wa Mataifa litakalokuwa na udhamini mkubwa.

Aidha Bi Rice amesema jeshi la Umoja wa Mataifa litakalowajumuisha wanajeshi kutoka nchi mbalimbali litaweza kuwaokoa wakaazi wa Darfur na kuleta amani ya kudumu katika eneo hilo.

Amesisitiza umuhimu wa kukabiliana na hali mbaya ya kibinadamu katika jimbo la Darfur.