1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Rice ziarani Mashariki ya Kati

25 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFc

Waziri wa nje wa Marekani,Condoleezza Rice ametoa wito wa kuwepo upatanisho kati ya Israel na madola ya Kiarabu.Alipozungumza na mawaziri wenzake kutoka nchi za Kiarabu,katika mji wa Asswan,nchini Misri,Rice alisema,hatua hiyo huenda ikasaidia kujenga uhusiano kati ya Israel na Wapalestina.Miongoni mwa masuala yaliojadiliwa katika mkutano uliohudhuriwa na mawaziri wa nje wa Misri,Saudi Arabia,Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE na Jordan,ni ule utaratibu wa amani uliopendekezwa na Waarabu hapo mwaka 2002. Kuambatana na mpango huo uhusiano na Israel utarekebishwa na badala yake,Israel irejee kwenye mipaka ya mwaka 1967.Lakini pendekezo hilo lilikataliwa na Israel wakati huo.