1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO: Talat Sadat avuliwa ulinzi wa bunge

6 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD5a

Mpwa wa kiongozi wa Misri aliyeuwawa Anwar Sadat amepoteza ulinzi wake wa bunge baada ya kulitaja jeshi kuhusika na kifo cha rais Sadat miaka 25 iliyopita.

Talat Sadat mwenye umri wa miaka 52 amevuliwa ulinzi huo kufuatia ombi lililowaslishwa na muongoza mashataka wa jeshi.

Uamuzi huo unaifungulia mlango kesi dhidi ya Sadat, ambaye ni mbunge wa chama kidogo cha upinzani cha Ahrar.

Marehemu Anwar Sadat aliuwawa na mwanamgambo wa kiislamu manmo Oktoba 6 mwaka wa 1981, wakati alipokuwa akikagua gwaride la heshima kusherehekea maadhimisho ya mwaka wa 1973 ya tangazo la vita dhidi ya Israel.