1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO:magazeti yagoma kufanya kazi

7 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Hk

Magazeti 23 ya watu binafsi na ya upande wa upinzani leo yamegoma kuchapisha habari ikiwa ni ishara ya kupinga hukumu zilizotolewa kwa wandishi habari nchini Misri.

Wandishi habari tisa pamoja na wahariri wa magazeti kadhaa wamehukumiwa vifungo jela ama adhabu ya kulipa faini kutokana na madai ya kuchapisha habari bandia , kuwakashifu viongozi wa chama kinachotawala na kueneza uvumi.

Miongoni mwa wahariri hao ni bwana Ibrahim Eissa aliehukumiwa kwa kueneza kilichoitwa habari za hatari juu ya afya ya rais Hosni Mubarak.

Hivi karibuni kulikuwa na uvumi kwamba hali ya afya ya rais Mubarak ilikuwa mbaya.