1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO:Misri kutuma jeshi Darfur

28 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6G

Misri imejitolea kutuma wanajeshi katika jimbo la mgogoro la Darfur nchini Sudan kuongeza nguvu kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa Afrika ambacho kimeshindwa hadi sasa kumaliza vurugu.

Waziri wa mambo ya nje wa Misri Ahmed Abul Ghiet amesema Misri imeufahamisha Umoja wa mataifa kwamba iko tayari kutuma wanajeshi 750 na kiasi cha waangalizi 100 wakijeshi kama sehemu ya wanajeshi 3000 wa Umoja wa mataifa watakaopelekwa Darfur kukipa nguvu kikosi cha Umoja wa Afrika.

Hatua hii inafuatia serikali ya Khartoum kukubali mwezi huu wanajeshi wa Umoja wa mataifa kupelekwa kwenye jimbo la Darfur kukomesha vita.

Wanajeshi hao watasaidia katika kutoa mahitaji muhimu ya kijeshi.