1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO:Misri ni moja ya nchi zinazokandamiza uhuru wa vyombo vya habari

3 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5J

Leo ni siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani na uchunguzi unaonyesha kwamba bado kuna ukandamizaji wa uhuru huo katika nchini nyingi na Misri imetajwa kuwa mojawapo.

Hapo jana Mahakama nchini humo imemhukumu kifungo cha miezi sita jela mwandishi habari wa kituo cha Aljazeera kwa kutaarisha filamu inayoonyesha unyanyasaji wa polisi.

Howayda Taha alishtakiwa kwa kuiharibia sifa Misri.

Makundi ya kutetea haki za binadamu nchini humo yameishutumu mahakama kwa kukiuka kanuni za kimataiafa zinazotambulika kuhusu utendaji wa haki katika kesi.Aidha makundi hayo yameikosoa Misri kwa kuvitendea kinyume vyombo vya habari.