1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO:Uchaguzi wa wabunge waendelea

11 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBso

CAIRO

Uchaguzi wa wabunge katika bunge dogo nchini Misri Shura unaendelea.Uchaguzi huo unashirikisha chama tawala cha Rais Hosni Mubarak na chama kikuu cha upinzani cha Muslim Brotherhood.Chama cha Muslim Brotherhood kinashiriki kwa mara ya kwanza na kuwasilisha wagombea 19 huku serikali ikiwasaka wafuasi wake.Polisi wa kupambana na ghasia walijihami na kushika doria kwenye kituo cha kupinga kura cha Manshiyat al Qanater mjini Giza.Mgombea wa Muslim Brotherhood Sayeed Saleh anagombea nafasi katika kituo hicho.Polisi hao waliwalazimisha wapiga kura kuondoka kituoni. Wabunge 176 pekee wa Shura wanachaguliwa moja kwa moja kwa muhula wa miaka sita na wengine 88 waliosalia wanachaguliwa na rais.Wagombea 587 wanawania nafasi 88 katika majimbo 24.Vyama vya upinzani vya al Wafd na Nasseria vinasusia uchaguzi huo.