1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO:Waislamu kubadili dini bila vikwazo

24 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBfj

Mshauri rasmi wa kidini nchini Misri anatangaza kuwa waislamu nchini humo wana uhuru wa kubadili dini yao kwani ni suala binafsi.Mufti kuu Ali Gomaa aliyeandika makala kwenye gazeti la Washington Post kubadili dini ya mtu bila sababu za msingi hakukubaliki.Kwa mujibu wa maandiko ya kidini jambo hilo linaadhibiwa na mwenyezi Mungu.

Katika jamii nyingi za kiislamu hatua ya kubadili dini huenda ikasababisha adhabu kali kutolewa kwa mhusika.

Nchini Misri juhudi za kubadili dini kutoka uislamu hadi nyingine zinakatizwa na hatua ya serikali ya kutotambua mabadiliko yale kwenye stakabadhi rasmi.wakati mwingine wahusika wanaadhibiwa kwa kifungo.

Kauli hii mpya inasisitiza kuwa hatua ya kubadili dini kutoka uislamu hadi nyingine inakubalika endapo haitaathiri maadili ya jamii.