1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAIRO:Wapinzani wasusia kikao cha bunge

19 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCHW

Wabunge wa upinzani nchini Misri wanasusia majadiliano kuhusu marekebisho ya katiba yanayoandaliwa bungeni yanayolenga kumpa Rais Hosni Mubarak madaraka zaidi.Rais Mubarak anaazimia kubadilisha vipengee 34 vya katiba ya nchi kama sehemu ya mabadiliko ya kiuchumi yaliyo na misingi ya demokrasia.Upande wa upinzani ambao ni robo ya wabunge wote nchini Misri wanapinga mabadiliko hayo na kudai kuwa yatabana kufanyika kwa uchaguzi vilevile kumpa madaraka makubwa rais kwa madhumuni ya kuwakandamiza wapinzani wake.

Mabadiliko hayo yanatokea wakati Marekani iliyo mwandani wa Misri inapunguza shinikizo dhidi yake ili kudumisha demokrasia.Uongozi wa Rais Bush ulilipa kipa umbele suala la kudumisha demokrasia miaka miwili iliyopita lakini kubadili mfumo baada ya Misri kuunga mkono juhudi za kustawisha amani katika eneo la Mashariki ya Kati.

Zaidi ya wabunge 100 wakiwemo wa chama kikubwa cha upinzani cha Muslim Brotherhood waliandamana ili kupinga mazungumzo hayo.