1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CALETONVILLE : Wafanyakazi 3,200 wa mgodi waokolewa

5 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7IS

Wafanyakazi wa mwisho kati ya 3,200 wameokolewa kwenye mgodi wa dhahabu nchini Afrika Kusini baada ya kunasa kwa zaidi ya masaa 24 chini ya ardhi ndani ya mgodi huo.

Wafanyakazi hao walikuwa wamenasa kilomita mbili chini ya ardhi kwenye mgodi wa dhahabu wa Elandsrand baada ya waya wa umeme kukatika na hiyo kupelekea kukatika kwa usambazaji wa umeme ndani ya mgodi huo.

Waziri wa Madini na Nishati wa Afrika Kusini Buyelwe Sonjica ameagiza kufungwa kwa mgodi huo ili uchunguzi ufanyike kujuwa chanzo cha ajali ambapo hakuna mtu aliejeruhi.

Sonjica anasema ili kwamba waweze kuchukuwa hatua yoyote ile kali iwapo mgodi husika utakaidi kuhusiana na suala la kuboresha hali yake ya usalama kwa hiyo wawe na madaraka ya kuchukuwa hatua yoyote ile.

Vyama vya wafanyakazi nchini Afrika Kusini vimesema ajali hiyo inafaa itumike kuwa wito wa kutadharisha juu ya ukosefu wa viwango vya usalama kwenye migodi.