1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cameron aahidi kuwasaka waliofanya ghasia

12 Agosti 2011

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ameahidi kuwasaka wale waliohusika na ghasia , uporaji wa mali na uchomaji majumba na magari , hali iliyotokea wiki iliyopita katika miji kadha ya Uingereza.

https://p.dw.com/p/12FPW
Kijana aliyejifunika uso akiburuza pipa la taka linaloungua moto katika kitongoji cha Hackney, mashariki ya London, Aug. 8, 2011.Picha: dapd

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ameahidi jana kuwasaka wale waliohusika na ghasia, uporaji wa mali na uchomaji moto majumba na magari, hali iliyotokea wiki iliyopita katika miji kadha nchini Uingereza.

Auschreitung in Großbritanien David Cameron 11.08.2011
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron akitoa maelezo bungeni jana. Ameahidi kuwachukualia hatua waliohusika katika ghasia.Picha: Dapd

Akizungumza bungeni, Cameron ameelezea mipango ya kuzuwia ghasia kama hizo kutokea tena hapo baadaye, ikiwa ni pamoja na kutoa mamlaka kwa polisi, kuliita jeshi kusaidia, na pengine hata kuweka hali ya kutotembea usiku. Mamia ya watuhumiwa wa uporaji kwa sasa wamefikishwa katika mahakama za Uingereza baada ya siku nne za ghasia za usiku. Utulivu umerejea katika miji mikubwa ya nchi hiyo na polisi 16,000 wataendelea kuwapo katika mitaa ya mjini London hadi mwishoni mwa juma