1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Cameroon yaenda uchaguzini

9 Oktoba 2011

Jamhuri ya Cameroon huko Afrika ya Magharibi hivi leo (09 Oktoba 2011) inaingia kwenye uchaguzi wa raisi na wabuge, ambapo raisi aliyepo madarakani, Paul Biya, anapewa nafasi kubwa ya kushinda.

https://p.dw.com/p/12oQI
Bendera ya Cameroon.
Bendera ya Cameroon.

Rais Biya ameitawala Cameroon kwa miaka 29. Upinzani unaonekana kugawanyika. Mgombea anayeonekana kumpa upinzani Rais Biy, ni John Fru Ndi, ambaye ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, Social Democratic Front. Kutokana na kupanda kwa bei za vyakula, Cameroon imekuwa ikijikuta kwenye maandamano mara kwa mara. Licha ya mapato ya rasilimali ya mafuta, nusu ya raia milioni 20 wa nchi hiyo wanaishi kwenye umasikini. Idadi ya wasio na ajira imefikia 60% kwa mujibu wa takwimu rasmi.

Mwandishi: Mohammed Khelef/ZPR Mhariri: Sekione Kitojo