1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAMP DAVID: Brown aendelea na ziara yake Marekani

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdc

Waziri mkuu wa Uingereza bwana Gordon Brown anaendelea na ziara yake nchini Marekani. Leo anatarajiwa kukutana na rais George W Bush huko Camp David.

Bwana Brown anajaribu kutafuta uugwaji mkono kuhusu mpango wa amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan na mazungumzo ya kibiashara ya shirika la kibiashara duniani, WTO, yaliyokwama.

Mazungumzo baina ya rais Bush na Gordon Brown yatakayohudhuriwa pia na mawaziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani na Uingereza, yanatarajiwa kugubikwa na tatizo la Irak.

Waziri mkuu Gordon Brown ameahidi kuuendeleza uhusiani kati ya Uingereza na Marekani lakini anatarajiwa kujiepusha na rais Bush kuhusina na swala la Irak.