1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAPE TOWN: Rais wa zamani mkaburu nchini Afrika ya kusini, Pieter Willem Botha afariki dunia

1 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCx5

Rais wa zamani wa Afrika ya kusini, Pieter Willem Botha amefariki dunia nyumbani kwake katika eneo la Cape, mgharibi mwa nchi akiwa na umri wa miaka 90. Botha aliotajwa´´ mamba kubwa ´´kutokana na sera zake za kuwakandamiza watu, aliiongoza nchi wakati wa utawala wa wazungu waliowachache kutoka mwaka 1978 hadi 1989. Alipuuza lawama za jumuiya ya kimataifa juu ya sera zake za ubaguzi wa rangi na makabila,Apartheid. Na hata baada ya kustafu, aliendelea kuwa na msimamo wake huo na kukataa kuripoti mbele ya tume ya ukweli na maridhiano ya taifa kuelezea juu ya tuhuma za ukiukaji wa haki za binaadamu zilizokuwa zikimkabili.