1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAPE TOWN : Serikali kuburuzwa tena mahkamani

16 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBYp

Wanaharakati wa Afrika Kusini wamesema hapo jana kwamba wanapanga kuiburuza serikali mahkamani kwa mara nyengine tena kutokana na mkakati wake wa virusi vya HIV na kusema kwamba kutimuliwa kwa naibu waziri wa afya anayeheshimika kumesababisha hofu na woga.

Kundi la Treatment Action Campaign ambalo ni kundi la wapiga debe wa UKIMWI lenye ushawishi mkubwa kabisa nchini Afrika Kusini lilishinda hukumu ya Mahkama ya Katiba hapo mwaka 2002 ilioilazimisha serikali kutowa madawa dhidi ya UKIMWI katika hospitali za taifa.

Kundi hilo limesema hivi sasa linataka mahkama kuu kuilazimisha idara ya afya ya taifa kuruhusu vituo vya matibabu nchini kote kuanzisha utaratibu wa matibabu katika mipango yake ili kuzuwiya maambukizi ya HIV kutoka kwa mama kwenda kwa watoto.