1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CAPE TOWN.Watu 20 wauwawa kwenye ajali

13 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCtA

Takriban watu 20 wameuwawa karibu na mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini katika ajali mbaya iliyohusisha kugongana kwa treni na lori lililokuwa limewabeba wafanyakazi wa shambani katika kivukio cha reli kwa mujibu wa shirika la habari la Afrika Kusini.

Msemaji wa shirika linalo shughulika na maswala ya dharura bwana Chris Botha amesema watu hao wamefariki katika ajali iliyotokea katika eneo la Somerset magharibi mwa Cape town.

Watu sita walionusurika wako katika hali mahututi.