1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Caracas. Che Guevara akumbukwa.

9 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HM

Watu katika nchi kadha za Latin Amerika wamekuwa wakiadhimisha kumbukumbu ya kiongozi wa kimapinduzi Che Guevara, miaka 40 baada ya kukamatwa kwake na kuuwawa. Che Guevara aliuwawa nchini Bolivia katika mwaka 1967 wakati akijaribu kujenga uasi dhidi ya nchi hiyo. Tangu kufa kwake, muasi huyo mwanamapinduzi mzaliwa wa Argentina amejipatia heshima ya mtu maarufu duniani, hususan kwa watu masikini na wale wanaokandamizwa katika mataifa yanayoendelea.

Marais wa Bolivia na Venezuela wamemsifu Che kuwa ni nguvu ya uhamasishaji ambayo haiwezi kuzimwa. Maelfu ya watu walihudhuria maadhimisho katika eneo alipozikwa nchini Cuba. Eneo hilo lipo katika eneo linalojulikana kama Santa Clara, ambako Che alipigana katika vita muhimu ya kuikomboa Cuba. Katika taarifa , kiongozi wa kimapinduzi nchini Cuba Fidel Castro amesema Che alipanda mbegu za kujitambua kijamii katika eneo la Latin America.