1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Caracas. Rais wa Iran aanza ziara Amerika ya kusini.

14 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCar

Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad , amewasili nchini Venezuela mwanzoni mwa ziara yake ya mataifa ya Amerika ya kusini.

Ziara ya Ahmedinejad itajumuisha nchi za Ecuador, Bolivia na Nicaragua, ambazo zote zinadhibitiwa na serikali za mrengo wa shoto ambazo zinapinga sera za serikali ya Marekani.

Ziara hiyo inaonekana kuwa ni juhudi za kutafuta kuungwa mkono wakati Iran inakabiliana na mbinyo wa jumuiya ya kimataifa kutoka Marekani na umoja wa Ulaya kuhusiana na mpango wake wa kinuklia.

Iran inadai kuwa mpango wake wa kinuklia ni kwa matumizi ya amani, lakini wapinzani wake wanasema ni mpango wa siri wa kutengeneza silaha za kinuklia.