1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CARACAS: Waandamanaji waunga mkono kituo binafsi RCTV

20 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0P

Maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Venezuela,Caracas kupinga mipango ya Rais Hugo Chavez ya kutaka kukifunga kituo cha televisheni cha kibinafsi RCTV kinachoshirikiana na upande wa upinzani.Rais Chavez amekituhumu kituo hicho kuwa kiliunga mkono jeribio la kutaka kumpindua hapo mwaka 2002.Sasa Chavez anataka kuwa na kituo kitakachoongozwa na serikali badala ya kuwepo kituo hicho cha binafsi.Waandamanaji lakini wanasema,mpango huo ni pigo kwa udemokrasia nchini humo.