1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CARACAS:Chavez ataka nadharia ya kisoshalisti mashuleni

18 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOo

Rais Hugo Chavez wa Venezuela ametishia kuzifunga shule za binafsi nchini humo iwapo zitakaidi kuingiza katika mitaala ya masomo nadharia ya kisoshalisti ya nchi hiyo.

Chavez amezitaka shule zote kuingiza somo jipya katika mtaala kuanza mwaka huu, somo ambalo amedai litasaidia kuimarisha umoja na ushirikiano.

Hata hivyo wazazi wengi wameonesha wasi wasi juu ya mtaala huo mpya ya kwamba utawatumbukiza watoto wao katika kasumba ya kikoministi.

Chavez amesema kuwa serikali iliyopita haikutoa umuhimu katika sekta ya elimu na kwamba elimu yenye nadhari za kibepari inasambaratisha thamani ya utu.