1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Caracass. Chavez atishia kutaifisha mabenki.

5 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4m

Rais wa Venezuela Hugo Chavez anatishia kutaifisha benki za binafsi nchini humo pamoja na kampuni kubwa kabisa nchini humo la kuzalisha chuma cha pua.

Hii inafuatia uamuzi wake kuchukua uendeshaji wa makampuni makubwa ya mafuta mapema wiki hii.

Chavez amesema kuwa mabenki na kampuni la chuma cha pua la Ternium-Sidor yanaweza tu kuepuka kutaifishwa iwapo watakwenda umbali kuweza kuangalia kile alichosema kuwa ni maslahi ya taifa.

Amesema kuwa benki zinapaswa kulenga katika kugharamia sekta ya viwanda badala ya kutafuta kupata faida kubwa.

Chavez ameuita mkakati wa kutaifisha makampuni muhimu , kuwa ni sehemu ya kipindi cha mpito nchini Venezuela kuingia katika mfumo wa kisoshalist.