1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CARLETONVILLE:Wafanyikazi 1500 waokolewa Afrika Kusini

4 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ib

Zaidi ya wachimba mgodi 1500 wameokolewa katika operesheni ya usiku kucha huku juhudi zikiendelea kuokoa mamia ya wengine waliosalia.Wachimba mgodi 3200 walinasa hapo jana katika mgodi wa dhahabu wa Elandsrand pale bomba la hewa lilipopasuka na kudondoka jambo lililosababisha uharibifu mkubwa kwa mujibu wa maafisa wa kampuni hiyo.

Wengi ya wahudumu hao walitatizika na kunasa wakiwa umbali wa kilomita moja u nusu chini ya ardhi na kulazimika kurejeshwa juu.

Yapata wahudumu 340 wamenasa chini zaidi katika eneo lililo na umbali wa kilomita alfu 3.Asubuhi ya leo zaidi ya 1500 waliokolewa kulingana na afisa mmoja wa kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa mgodi huo Stan Bierschenk wengi ya wafanyikazi hao waliokolewa walilalamikia uchovu kwasababu ya joto.Hakuna majeruhi wowote walioripotiwa na hakuna hatari ya dharura kwa wafaynikazi wote wa mgodi huo.

Shughuli za uokozi zinatarajiwa kukamilika mchana huku msemaji wa Mgodi huo wa Elandsrand akiongeza kuwa utafungwa ili uchunguzi wa ajali hiyo kufanyika.