1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

CDU-FDP: Mwanzo mpya au Mwisho

28 Septemba 2009

<p>Angela Merkel amefanikiwa katika matarajio ya lengo lake, anaweza kuunda serikali ya mseto ya rangi nyeusi na njano.

https://p.dw.com/p/JqYc
Supporters of the Christian Democratic Party, CDU, celebrate with Chancellor Angela Merkel, center, after the German general elections in Berlin, Sunday, Sept. 27, 2009. (AP Photo/Franka Bruns)
Mashabiki wa chama cha CDU wakishangilia ushindi pamoja na Kansela Angela Merkel katikati.Picha: AP
Lakini  hii  hata  hivyo  si  kutokana  na mafanikio  yake  binafsi, badala  yake  ni  kutokana  na hali  mbaya  ya  kuporomoka  kwa  chama  cha  SPD.  Ndio sababu  anafikiria  Marc  Koch  katika  maoni  yake   kuwa Angela  Merkel   atakuwa  kiongozi  wa  muda  wa  serikali.

Ushindi wake hauwezi  kubadili mkondo. Huu ni mwanzo wa kuelekea  mwisho, kwani chama cha Kansela Angela Merkel pamoja na  kubakia madarakani kimepata matokeo mabaya kabisa kuwahi kuyashuhudia tangu kuundwa Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani. Huenda  Kansela akahitaji miaka miwili au pengine  mitatu kurekebisha hali hiyo. Matumaini yaliopo pamoja na hayo  si kwa sababu tu  sasa wahafidhina wanatamaa ya  kuleta  mageuzi yaliokwama  wakati wa serikali ya mseto na Wasocial democrats,  bali chama chake CDU/CSU kiliamua kuunda serikali ya mseto na FDP.

Waliberali wamepata matokeo bora kabisa katika historia yao katika uchaguzi wa Shirikisho. Bila shaka  FDP itatarajiwa kuyalipia matokeo hayo yawe ya kivitendo badala ya ahadi za maneno matupu.

Westerwelle und Merkel
Guido Westerwelle na Angela Merkel baada ya matokeoPicha: AP

Sera yao ya kukabiliana na msukosuko wa  fedha na kiuchumi na kuhusiana na  kodi, ni mambo yaliowavutia wapiga kura  na kuwapa pigo CDU na SPD. Kinachosubiriwa ni kuona kama wapiga kura waliokipa imani hiyo watashuhudia ahadi hizo zikitekelezwa au la.

Vyama vya umma  kwa hivyo vimepambana  katika uchaguzi, lakini hapakutokea hali ya kuvunjika  moyo  wapiga kura na kampeni kama safari hii. Walichokuwa wakitafuta ni mustakbali wa uhakika na wenye kuambatana na  hali halisi ilivyo. Muungano  wa vyama vikubwa  Wahafidhina wa Christian Democrats na Wajamaa Social Democrats ulishindwa  kuwapa matumaini  katika kipindi cha miaka minne  iliopita ya serikali yao ya mseto.

 Taifa hili sasa limo katika utaratibu wa vyama vitano bungeni.

Kwa upande mwengine miaka minne ijayo  itakuwa wakati wa kutafakari kwa  Steinmeier na  SPD, kutokana na  umaarufu uliotokeza kwa chama cha mrengo wa shoto Die Linke. Na kwa muungano mpya wa Bibi Angela Merkel kinachosubiriwa ni matokeo, la sivyo pengine kwake na CDU  utakuwa ni mwanzo wa kuelekea mwisho.

Mwandishi: Koch,Marc/ZR/S.Kitojo

Mhariri:M.Abdul-rahman