1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha CUF yasema mazungumzo na chama tawala cha CCM yamekwama

8 Agosti 2007

Mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea baina ya chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha CUF, na chama tawala cha CCM, yenye lengo la kumaliza kile kilichobatizwa jina la mpasuko wa kisiasa Zanzibar yamekwama.

https://p.dw.com/p/CH9u
Profesa Ibrahim Lipumba,mwenyekiti wa chama cha CUF
Profesa Ibrahim Lipumba,mwenyekiti wa chama cha CUFPicha: DW

Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba katika makao makuu ya chama hicho Buguruni mjini Dar es salaam mbele ya waandishi wa habari.

Mwandishi wetu Christopher Bhuke anaripoti zaidi kutoka Dar es salaam.