1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Demokratik Marekani kuamua juu ya uchaguzi wa Michigan na Florida

31 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/EAOg

WASHINGTON

Chama cha Demokratic nchini Marekani kinakutana baadae leo hii kuamua hatma ya uchaguzi wa majimbo ya Florida na Michigan ambayo matokeo yake hayakuhesabiwa katika chaguzi za awali za kuteua mgombea wa urais atakayewakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.Majimbo hayo mawili yaliondolewa kwenye uwakilishi kwasababu ya kufanya uchaguzi wake wa awali mwezi Januari hatua ambayo inakiuka sheria za chama cha Demokratic.Matokeo ya uchaguzi wa awali katika majimbo hayo yalimpa ushindi Hillary Clinton ambaye sasa anamatumaini kwamba chama kitabadili msimamo wake kuelekea majimbo hayo.Clinton anatarajia kwamba kamati ya wanachma 30 itabatilisha uamuzi wake wa awali na kuruhusu wajumbe kutoka majimbo ya Florida na Michigan washiriki kwenye uchaguzi katika baraza kuu la kitaifa la chama hicho mwezi Agosti ambalo litaamua nani ashikilie bendera ya chama hicho kati ya Clinton na Obama katika uchaguzi wa rais dhidi ya mgombea wa Republican John MaCcain.