1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha MDC Zimbabwe chasusia mikutano ya Baraza la mawaziri

20 Oktoba 2009

Licha ya chama cha MDC, cha waziri mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai, mawaziri wake kususia kuhudhuria mikutano ya baraza la mawaziri la nchi hiyo, hata hivyo, Rais Mugabe leo aliongoza mkutano wa baraza hilo.

https://p.dw.com/p/KBSG
Chama cha MDC cha Waziri mkuu Morgan Tsvangirai wa Zimbabwe,wasusia mkutanoPicha: AP

Mwenyewe Morgan Tsvangirai amekuwa akizitembelea Afrika Kusini na Msumbiji kuwaomba viongozi wa nchi za Kusini mwa Afrika wasaidie kuutanzua ugomvi ulioibuka sasa baina yake yeye na Chama cha rais Robert Mugabe, ZANU-PF. Utaratibu wa Zimbabwe wa kugawana madaraka baina ya vyama vilivokuwa hasimu kabla ya uchaguzi ni kama ule ambao uko huko Kenya hivi sasa baina ya Rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga.

Othman Miraji alizungumza na Prof. Wangari Maathai wa Kenya, mshindi wa zawadi ya amani ya Nobel, na alimuuliza vipi anavouona mzozo huu wa sasa wa huko Zimbabwe.