1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha SPD chakanusha kuelemea mrengo wa kushoto

22 Februari 2008
https://p.dw.com/p/DBS2

BERLIN:

Kiongozi wa chama cha Social Demokrats SPD nchini Ujerumani Kurt Beck amepuuza ripoti zinazosema kuwa chama hicho huenda kikavunja mwiko wa kihistoria kwa kushirikiana na chama cha Die Linke-kundi jipya linaloegemea mrengo wa kushoto na lililo na wakomunisti wa zamani.Uwezekano wa kuundwa serikali ya jimbo la Hesse kwa msaada wa chama cha mrengo wa kushoto,umezusha midahalo mikali katika chama cha SPD.Lakini Beck amesema, hakuna suala la kushirikiana na chama cha Die Linke lakini hakupinga moja kwa moja iwapo mgombea wa SPD Bibi Andrea Ypsilanti atakubali kura za Die Linke ili aweze kuchaguliwa kama waziri mkuu wa jimbo la Hesse.Uchaguzi uliofanywa mwishoni mwa mwezi wa Januari katika jimbo la Hesse umeingiza vyama vitano bungeni.Hakuna vyama vikuu vilivyopata wingi mkubwa wa kuweza kuunda serikali.