1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha Umma chajitoa kwenye uchaguzi Sudan

Josephat Nyiro Charo8 Aprili 2010

Hali ya kuaminika katika uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia nchini Sudan baada ya kupita miaka 25 inazidi kufifia licha ya jitihada za kuyashughulikia malalamiko ya vyama vya kisiasa nchini humo.

https://p.dw.com/p/MqYK
Rais Omar Hassan al Bashir akijiandikisha kwa ajili ya uchaguziPicha: picture alliance/dpa

Chama cha Umma Party kinachoongozwa na Sadek al-Mahdi aliyewahi kushika wadhifa wa Uwaziri mkuu katika Serikali ya Rais Omar Al Bashir,kinaelezwa kuwa ndio Chama kikuu cha upinzani nchini humo,kilitarajiwa kutangaza kujiondoa mapema katika uchaguzi huo ambao umekuwa ukilalamikiwa na vyama vya upinzani kuwa umegubikwa na hila na udanganyifu,huku malalmiko mengi yakitupiwa kwa tume ya taifa ya uchaguzi.

Kiongozi wa kitengo cha siasa wa Chama cha Umma Sarah Nugdalla amewaeleza makundi ya waandishi wa habari juu ya uamuzi huo,baada ya mkutano wa Chama hicho uliofanyika Omdurhan,karibu na mto Nile katika jiji la Khartoum.

Uwezekano wa kufanyika uchaguzi huo katika siku tatu zijazo,ulianza kutiliwa shaka ya kufanyika baada ya Chama kingine cha upinzani cha SPLM,kuelezea msimamo wa kususia uchaguzi huo,ambapo pia waangalizi wa kimataifa kutoka jumuiya ya Ulaya kutangaza kujiondoa katika jimbo la Darfur kufuatia hali ya usalama kuwa mbaya.

Hapo kabla waangalizi kutoka Umoja wa Afrika wakiongozwa na Rais wa zamani wa Ghana John Kuffour walitoa taarifa ya kuanza kwa mazungumzo na vyama hivyo juu ya uwezekano wa kuendelea na uchaguzi

o- tone

Umma Party kabla ya kutangaza kuususia uchaguzi huo,iliipa Serikali iliyo madarakani siku nne kuanzia tarehe 2 mwezi huu,iwe imefanyia marekebisho vipengele kadhaa vya uchaguzi,ili waweze kushiriki katika kinyang´anyiro hicho,ambacho Chama hicho kiliwahi kushinda katika Uchaguzi wa mwaka 1986,kabla ya kuondolewa madarakani na Rais wa sasa Omar Al Bashir.

Nugdalla alisema na hapa ninamnukuu; Kitengo cha Siasa cha Chama chetu kilijadili suala hili kwa zaidi ya siku mbili,tumesikiliza pande zote juu ya hili,na mwisho tumekubaliana kwamba maombi yetu ya kusogezwa mbele uchaguzi hayakukubaliwa´´ Mwisho wa kumnukuu.

Rais Omar Al Bashir anatarajiwa kushinda uchaguzi huo uliopangwa kufanyika tarehe 11-13 mwezi huu,licha ya kutakiwa kutakiwa kufikishwa katika Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita,ambapo tume ya uchaguzi imesisitiza uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa,licha ya malalamiko ya vyama vya kisiasa dhidi ya tume hiyo.

Umma Party ilitoa masharti nane ambayo walitaka yatimizwe kabla ya kufanyika uchaguzi huo,lakini wameeleza kuwa ni ombi moja tu kati ya hayo linalohusu gharama za uchaguzi ndio lililotimizwa na Serikali kufikia tarehe 6,ambapo kwa mujibu wa Nugdullah kiongozi wao wa Umma,Sadeq al Mahdi amepewa nafasi ya kufanya maamuzi kwa maslahi ya taifa kwa kutangaza kujiondoa katika uchaguzi huo.

Vyama viwili vingine vimetajwa na Mahdi kuwa vimepanga kufuata msimamo wa Umma Party na kujiunga na Chama cha SPLM kilichojiondoa mapema kushiriki katika chaguzi za Kaskazini,isipokuwa kimetangaza kushiriki katika majimbo wanayoungwa mkono zaidi ya Blue Nile na Kordofan ya Kusini.

Mwandishi; Ramadhan Tuwa/ AFP/AFPE/

Mhariri: Sekione Kitojo.