1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama cha upinzani Taiwan chapata viti vingi bungeni

13 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Coxs

TAIPEI:

Chama cha upinzani nchini Taiwan cha Kuomintang,KMT kimeshinda uchaguzi wa bunge uliofanyika jana nchini humo .Tume ya uchaguzi nchini humo KMT ambacho kinapendelea uhusiano wa karibu na Beijing kimepata viti 81 kati ya vyote 113 vya bunge hilo. Rais Chen Shui-bian amekubali kushindwa na kutangaza kujiuzulu kama mwenyekiti wa chama cha Demokratic Preogressive. Wachunguzi wanaona uchaguzi wa bunge kama kigezo cha uchaguzi mkuu wa urais wa taiwana utakaofanyika katika kipindi cha miezi miwili kutoka sasa.