1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama kikuu cha upinzani Kenya chapanga mkakati mpya

19 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cugm

NAIROBI: Chama cha upinzani nchini Kenya ODM kimesema, Ijumaa ndio ilikuwa siku ya mwisho ya kufanywa maandamano mitaani,kupinga matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi uliopita ambao upinzani unasema ulifanyiwa udanganyifu na chama tawala.

Kwa mujibu wa chama cha upinzani ODM,sasa kimepanga kususia biashara za matajiri wanaohusika na serikali na vile vile kitajiimarisha kwa hatua zitakazochukuliwa katika bunge la Kenya.

Kiasi ya watu 700 wameuawa katika machafuko ya upinzani yaliyozuka kufuatia uchaguzi wa Desemba 27.Rais Mwai Kibaki alitangazwa mshindi wa uchaguzi huo kwa wingi mdogo mno,dhidi ya kiongozi mkuu wa upinzani Raila Odinga.