1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama tawala CCM nchini Tanzania kimeridhia kuundwa serikali ya mseto visiwani Zanzibar

16 Februari 2010

<p>Halmashauri ya taifa ya chama tawala cha Mapinduzi, CCM, huko Tanzania ilikutana kwa faragha kwa siku mbili huko Dodoma hadi jana usiku.

https://p.dw.com/p/M32v
Na kati ya mambo yaliokabiliwa na kikao hicho kuyajadili ni hali ya kisiasa Visiwani Zanzibar baada ya Baraza la wawakilishi visiwani humo, kwa kauli moja, kulikubali pendekezo la kuundwa serikali ya umoja wa kitaifa, na pia ripoti ya kamati ya chama hicho ilioundwa kusuluhisha tofauti zilizochomoza kati ya wabunge wa chama hicho baina ya wale wanaotajwa kupinga ufisadi na wale wanaotuhumiwa kuuendeleza ufisadi.

Othman Miraji amezungumza kwa njia ya simu na John Chiligati ambaye ni katibu mwenezi na itikadi wa Chama cha CCM. Kwanza anaelezea hivi kilichokubaliwa huko Dodoma jana kuhusu maridhiano ya Zanzibar...

Mahojiano :Othman Miraji/John Chiligati

Mhariri: Mohamed Abdulrahman