1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama tawala Ufaransa chashindwa, katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Nyanza, Halima17 Machi 2008

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, anatarajiwa kwa kiasi kikubwa kubadili mtindo wake wa uongozi, baada ya kushindwa vibaya katika uchaguzi wa Mabaraza ya miji uliofanyika jana.

https://p.dw.com/p/DPoJ
Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy, ambaye chama chake kilishindwa, katika uchaguzi wa jana wa serikali za mitaa nchini humo.Picha: picture-alliance/ dpa

Lakini hata hivyo, Wasaidizi wake wameondoa uwezekano wowote wa kufanyiwa marekebisho ya kiuchumi au baraza la Mawaziri.

Ikiwa ni miezi 10 tu, tangu Rais Sarkozy aingie madarakani, wapiga kura wengi wanahisi kwamba hawasaidii ama kuwalinda kutokana na kupanda kwa ughali wa maisha na kuhisi kuwa amejikitia zaidi katika mambo yake binafsi ikiwemo kufunga ndoa na mwanamitindo wa zamani Carla Bruni.

Chama cha Upinzani cha Wasosholisti kimefanikiwa kudhibiti zaidi ya miji 20 kutoka katika chama cha Rais Sarkozy cha mrengo wa kulia, cha UMP katika uchaguzi uliofanyika jana.

Aidha chama hicho cha Wasosholisti, pia kimeushikilia mji mkuu wa nchi hiyo, Paris.

Kuhusu Chama tawala cha UMP kuweza kushikilia mji wa Marseille ambao ni wa tatu kwa ukubwa nchini Ufaransa, hakuwezi kuficha ukweli wa jinsi chama hicho kilivyoshindwa nchi nzima katika jaribio hilo la kwanza dhidi ya umaarufu wa Rais Sarkozy tangu ashinde mwei mei mwaka jana.

Chama cha Kisosholist kimesema kuwa matokeo ya kura hiyo yanalenga hasa uchumi unaodhorota wa wa nchi hiyo, wakati viongozi wa UMP wanasema matokeo hayo ya kura yanaonesha kuwa wapiga kura wanataka serikali izidishe kufanyia marekebisho mipango mbalimbali ikiwemo katika afya, elimu na mpango wa akiba ya uzeeni.

Lakini hata hivyo wasaidizi wa Rais Sarkozy wanasema upigaji kura huo ni kama kuchochea mabadiliko kwa jinsi Rais huyo anavyofanya kazi yake.

Vyombo vya habari vinashauri kuwa Rais Sarkozy aanze kazi kwa kuichangamsha timu yake.

Wanasiasa wa uipinzani wanaeleza kuwa matokeo hayo ya uchaguzi huo wa Mabaraza ya miji yanaonesha jinsi wapiga kura wanavyohofia kupanda kwa gharama za maisha, hivyo wamesema Rais Sarkozy anapaswa kubadili sera zake.

Adha wachamuzi wa masuala ya kisiasa nchini humo, wameeleza kuwa matokeo hayo ya uchaguzi huo wa mabaraza ya miji, yamepinguza haiba ya Rais huyo wa Ufaransa.