1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Chama tawala Zimbabwe chashindwa kudhibiti bunge

Mohamed Dahman26 Aprili 2008

Chama tawala cha Rais Robert Mugabe nchini Zimbabwe kimeshindwa kujipatia udhibiti wa bunge nchini humo baada ya kuhesabiwa upya kwa baadhi ya kura za uchaguzi wa bunge uliofanyika tarehe 29 mwezi wa Machi mwaka huu.

https://p.dw.com/p/Dp6e
Morgan Tsvangirai kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha MDC.Picha: AP

Matokeo yaliotolewa leo hii yanaonyesha kushindwa kwa chama hicho tawala cha ZANU- PF kwa mara ya kwanza kabisa katika historia yake ya miaka 28 Mugabe alishinikiza kuhesabiwa upya kwa kura baada ya chama cha upinzani cha MDC kushinda wingi wa viti bungeni katika uchaguzi huo.Chama cha ZANU- PF kimekuwa kikiwashutumu maafisa wa uchaguzi kwa kupokea hongo ili kushusha idadi ya kura za chama hicho.

Kiongozi wa chama cha upinzani MDC Morgan Tsvangirai akiungwa mkono na Marekani amekuwa akidai kwamba ameshinda uchaguzi huo moja kwa moja ukiwemo ule wa rais ambao matokeo yake hadi hivi sasa hayakutangazwa.

Tume ya Uchaguzi ya Zimbabwe ZEC imesema kwamba majimbo 14 kati ya 23 kura zake zilizohesabiwa upya hadi sasa matokeo ya awali yamethibitishwa kuwa sahihi.

Suala la uchaguzi wa Zimbabwe linatazamiwa kujadiliwa katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo Ijumanne ijayo..