1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Champions League: nani atatinga fainali?

Sekione Kitojo
1 Mei 2017

Timu nne zinatafuta tiketi mbili za kutinga fainali ya Kombe la kifahari la Champions League itakayoandaliwa mjini Cardiff Juni 3

https://p.dw.com/p/2cC6m
Spanien Fußball Primera Division Real Madrid - Atletico Madrid
Picha: picture-alliance/dpa/D. Ochoa De Olza

Nusu  fainali  ya  kombe  la Champions  league   barani Ulaya  inafanyika Jumanne na  Jumatano  ambapo mabingwa watetezi Real Madrid inakabana koo  na  majirani  zao Atletico  Madrid. Real  ni  timu  pekee  ambayo  imeizuwia Atletico  Madrid  kuongeza  ubingwa  wa   Champions League  katika  mafanikio  yake  chini  ya  Diego Simeone na  kwa  mwaka  wa  nne  mfululizo  kikosi   cha "Rojiblancos" kimezuwia  njia  ya  Atletico  kupata  taji  hilo la  Ulaya.

Atletico  chini  ya  kocha  wake raia wa  Argentina Diego  Simeone imeweza  kuvifungisha  virago  vigogo  vya soka la  Ulaya  , kama  AC Milan, Chelsea, Juventus , Bayern Munich ,  na  mara  mbili Barcelona, lakini wameshindwa  mara  kadhaa  na  majirani  zao Real madrid. Mchezo  mwingine  wa  nusu  fainali  utafanyika Jumatano  kati  ya  Monaco inayopambana  na  Juventus Turin.

Mwandishi: Sekione  Kitojo / rtre / afpe / dpae
Mhariri: Iddi Ssessanga