1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Changieni kumsaka Kony-UN

15 Juni 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Majeshi ya Umoja wa Afrika sambamba na Wanajeshi wa Marekani wanaosaidia kumsaka Joseph Kony na kundi lake la LRA wanahitaji msaada ili kuweza kufanikisha jukumu hilo.

https://p.dw.com/p/15FkE
Ban Ki-moon
Ban Ki-moonPicha: Reuters

Ameomba wanachama wa Umoja huo kuchangia jukumu hilo. Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa jana, wanachama wote wa umoja huo wanaombwa kuchangia mahitaji yote muhimu.

Wanajeshi hao hawana vitendea kazi, chakula, usafiri na mafunzo ya kutosha ambayo ni mahitaji muhimu kufikia lengo la kumtia nguvuni Kony na kuliteteketeza kundi lake la LRA.

lord resistance Army-Uganda ** FILE ** Members of Uganda's Lord's Resistance Army are seen as their leader Joseph Kony meets with a delegation of Ugandan officials and lawmakers and representatives from non-governmental organizations, on July 31, 2006 in the Democratic Republic of Congo near the Sudanese border. The Lord's Resistance Army is made up of the remnants of a rebellion that began in 1986. The rebels are accused of attacks on civilians and aid workers in neighboring Congo and Sudan, where they sought refuge as the Ugandan army gained an upper hand in northern Uganda. (AP Photo) ** zu unserem Korr **
Lord Resistance Army - UgandaPicha: AP Photo

Changamoto za kupambana na LRA

Katibu Mkuu Ban Ki Moon amesema kuwa changamoto nyingine ni kuhakikisha kuwa mataifa na majeshi yaliyojirani na eneo linaloathirika na wanamgambo wa LRA kushiriki kikamlifu kumsaka kiongozi huyo wa waasi ili sheria ifuate mkondo wake.

Mpaka sasa ni kipindi cha miaka zaidi ya 20 Josephy Kony akiwa msituni anahusishwa na mauaji ya maelfu ya watu na watoto wanatumika kama askari, wapagazi na watumwa wa ngono.

Ushuhuda wa Grace Akallo

Grace Akallo ambaye miongoni mwao aliingizwa katika kundi la waasi la LRA mwaka1996 miezi saba baadae alifanikiwa kutoroka anasema wazi kuwa alipokuwa huko alipata mafunzo ya kina ya kutumia silaha kubwa kubwa za kivita kama vile AK 47 na aliona rafiki zake wakishurutishwa kuwaua wazazi wao bila ya woga wowote.

"Nilikuwa na miaka13, walitushurutisha kuwauwa watu sita na kurudi na vichwa vyao na tulifanya hivyo, nilijifungua mtoto huku nabeba bunduki begani."

Ripoti iliyotolewa hapo awali ilibainisha kuwa kati ya Julai 2009 na Februari 2012 kikundi hicho kimewaua watoto 591 ambapo wasichana ni 268 na wavulana 323 katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya kati tu.

Msemaji wa Jeshi la Uganda Kanali Felix Kulahije anasema LRA sio tatizo la nchi moja. "Tatizo la LRA ni la ukanda mzima si la Uganda pekee ndiyo maana Marekani imetuunga mkono kupambana nalo kundi hili la kigaidi."

Joseph Kony
Joseph Kony

Maombi ya Baraza la Usalama

Majeshi ya Umoja wa Afrika yalianza kumsaka Josephy Kony Mwezi Machi mwaka huu wakiwa na kikosi cha askari 5000 wakipatiwa mafunzo maalumu kutoka wanajeshi wa Marekani.

Pia hapo awali Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliziomba nchi za Chadi, Jamhuri ya Afrika ya kati na Sudan kusaidia kufanikisha kukamatwa kwa Joseph Kony na kikundi chake cha LRA.

Mwandishi:Adeladius Makwega/DPAE/AFPE/RTRE

Mhariri:Yusuf Saumu